Sera ya Faragha
WekaOrder ni huduma ya mtandaoni inayowasaidia wafanyabiashara wa Tanzania kufungua duka la mtandaoni na kupokea na kusimamia order. Sera hii inaeleza taarifa tunazokusanya, kwa nini tunazitumia, tunazihifadhi wapi na kwa muda gani, na haki zako. Inahusu website ya wekaorder.billybuilds.co.tz na app ya WekaOrder.
1. Sisi ni nani
WekaOrder ni huduma ya WEKA ORDER ENTERPRISES, jina la biashara lililosajiliwa BRELA (Na. 720428), inayoendeshwa na Billy Patrick, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa taarifa za wauzaji na wafanyakazi wao, WekaOrder ndiyo inayoamua jinsi zinavyotumika. Kwa taarifa za wateja wanaoagiza kwenye duka, muuzaji ndiye mwenye jukumu kwa wateja wake, na WekaOrder inazihifadhi kwa niaba yake ili order ikamilike.
2. Taarifa tunazokusanya
- Wauzaji: jina, namba ya simu, nenosiri, na barua pepe kama wameiweka (si lazima). Nenosiri halihifadhiwi kama lilivyo, bali kwa njia fiche isiyoweza kusomwa.
- Kuingia kupitia Google: muuzaji akichagua njia hii, Google inatupa jina lake, barua pepe yake na kitambulisho cha akaunti yake ya Google. Tunahifadhi kitambulisho hicho ili kumtambua anapoingia. Akifungua akaunti kupitia Google, barua pepe hiyo inakuwa barua pepe ya akaunti yake. Hatupati nenosiri lake la Google wala data nyingine za akaunti yake. Anaweza kuondoa muunganisho huu kwenye Akaunti yangu.
- Duka: jina, link ya duka, maelezo, mkoa, anwani, namba ya WhatsApp, link za mitandao ya kijamii, picha, bidhaa, bei na code za punguzo.
- Usajili (subscription): kiasi ulicholipa, njia ya malipo, reference na tarehe.
- Wafanyakazi (staff): jina na simu vilivyowekwa na mwenye duka, pamoja na nenosiri lao na barua pepe kama wameiweka.
- Wateja wanaoagiza: jina, namba ya simu, anwani ya kufikishiwa (ukichagua delivery), maelezo ya order, bidhaa ulizoagiza, code ya punguzo uliyotumia, reference ya malipo uliyotuma, na tangazo lililokuleta dukani (mfano link ya Instagram), kama lipo.
- Wageni wa maduka: tunahesabu ni watu wangapi wamefungua ukurasa wa kila duka kwa siku. Kwa hili hatutumii cookie wala kuhifadhi anwani ya IP. Tunatumia alama (hash) inayobadilika kila siku na kufutwa siku inayofuata, ili mtu mmoja asihesabiwe mara mbili siku moja. Muuzaji na WekaOrder wanaona jumla tu, si nani alitembelea.
- Customer care: ujumbe unaotuma kwa WekaOrder kupitia dashboard.
- WhatsApp inbox: duka likiunganisha namba yake ya WhatsApp Business (Cloud API), tunahifadhi ujumbe unaotumwa na kupokelewa, pamoja na jina na namba ya mteja anayeandika. Muuzaji akiunganisha WhatsApp Business app yake, tunahifadhi pia ujumbe anaoutuma kutoka kwenye app hiyo, historia ya chats zake na wateja mmoja mmoja ya hadi miezi 6 (kama ameruhusu kwenye app), na majina na namba za contacts zake za WhatsApp, ili inbox ionyeshe majina. Chats za groups hazihifadhiwi.
- AI msaidizi: muuzaji akibandika ujumbe wa mteja ili AI iandae cart na jibu, ujumbe huo unatumwa kwa mtoa huduma wa AI (kwa sasa Google Gemini) bila namba za simu wala barua pepe, na WekaOrder haiuhifadhi. Tunahifadhi maelezo ambayo muuzaji ameandika kwa ajili ya AI, na majibu 10 ya mwisho aliyoyarekebisha (yanaweza kuwa na jina la mteja), ili AI ifuate mtindo wake.
- Chat za AI: maswali ambayo mtu anaandika kwenye chat ya duka (muuzaji akiiwasha) au kwenye chat ya msaada ya ukurasa wa mwanzo, pamoja na ujumbe wa awali wa mazungumzo hayo, yanatumwa kwa mtoa huduma huyo huyo wa AI bila namba za simu wala barua pepe. WekaOrder haiyahifadhi; mazungumzo yanabaki kwenye browser ya mtu huyo hadi afunge tab.
- Arifa za simu: ukiwasha arifa za order, tunahifadhi anwani ya arifa ambayo browser ya kifaa chako inatoa, ili tukutumie arifa. Arifa ya ujumbe mpya wa WhatsApp inaonyesha jina la kwanza la mteja na mwanzo wa ujumbe wake.
- Taarifa za usalama: cookies za kuingia, alama (hash) ya kila browser uliyoingia nayo, hesabu ya nenosiri lililokosewa, na kumbukumbu za matukio muhimu (mfano akaunti ilipoingiwa, nenosiri lilipokosewa au kubadilishwa, au admin alipositisha duka).
3. Kwa nini tunatumia taarifa hizi
- Kuendesha duka lako, na kupokea, kusimamia na kuthibitisha order.
- Kumwezesha muuzaji kuwasiliana na mteja kuhusu order yake.
- Kumwonyesha muuzaji idadi ya wageni wa duka lake, na WekaOrder jumla ya wageni wa maduka yote.
- Kumsaidia muuzaji kuandaa cart na jibu kwa mteja kwa AI msaidizi, akichagua kuutumia.
- Kujibu maswali ya wateja kwenye chat ya duka kwa AI, na kuwapendekezea bidhaa za kuweka kwenye cart, muuzaji akiiwasha; na kujibu maswali kuhusu WekaOrder kwenye chat ya ukurasa wa mwanzo.
- Kuingia kwa usalama kwa barua pepe au namba ya simu, kutuma link ya kubadilisha nenosiri kwa barua pepe (au kwa WhatsApp, kama akaunti haina barua pepe na mwenye akaunti ameiomba), uthibitisho wa hatua mbili (MFA), kuzuia kwa muda akaunti ambayo nenosiri lake limekosewa mara nyingi, na kukujulisha kwa barua pepe (au kwa arifa, kama akaunti haina barua pepe) akaunti yako ikiingiwa kutoka browser mpya.
- Kusimamia usajili wa duka na malipo yake.
- Kujibu maswali ya customer care.
- Kulinda huduma dhidi ya udanganyifu na matumizi mabaya, na kutimiza matakwa ya sheria, kama kodi.
Hatuuzi taarifa zako. Hatuweki matangazo ya makampuni mengine kwenye WekaOrder, na hatutumii taarifa zako kwa matangazo ya mtu mwingine.
4. Nani anaona taarifa zako
- Muuzaji na wafanyakazi wake wanaona order za duka lao tu. Wafanyakazi wanaona order na malipo pekee, si mipangilio wala usajili wa duka.
- Admin wa WekaOrder anaweza kuona taarifa za maduka ili kutoa msaada na kulinda huduma.
- Chats za WhatsApp: muuzaji akitoa ruhusa (si lazima, na anaweza kuiondoa wakati wowote), admin wa WekaOrder anaweza kusoma chats za duka hilo ili kumpa muuzaji support na kuipa chat topic. Admin anaona tarakimu 4 za mwisho tu za namba ya mteja, lakini anaona jina na ujumbe wake. WekaOrder pia inaona jumla ya chats kwa kila topic, kwa maduka yaliyotoa ruhusa hiyo. Bila ruhusa hiyo, admin hawezi kuona chats hizo kwenye dashboard ya admin. Nakala kamili za akiba (backups) ambazo admin anaweza kupakua zina data yote, pamoja na chats na namba kamili, na zipo kwa ajili ya kurejesha huduma tu.
- Railway (Marekani) inaendesha server na database ya WekaOrder.
- Backblaze (Uholanzi) inahifadhi nakala za akiba (backups) za kila wiki. Zinasimbwa (encrypted) kabla ya kutoka kwenye server ya WekaOrder, kwa hiyo Backblaze haiwezi kuzisoma, na zinafutwa baada ya siku 30.
- Resend (Marekani) inatuma barua pepe za kubadilisha nenosiri.
- Huduma za arifa za browser (Google, Apple, Mozilla au Microsoft) zinapeleka arifa za order na za WhatsApp kwenye kifaa chako. Maudhui ya arifa yamesimbwa (encrypted), kwa hiyo huduma hizo haziwezi kuyasoma.
- Meta (WhatsApp): kama duka limeunganisha WhatsApp Cloud API, ujumbe wa WhatsApp unapita kwa Meta. Ndivyo ilivyo pia kwa mazungumzo yako na WekaOrder kwenye WhatsApp, kama link ya kubadilisha nenosiri. Muuzaji ambaye hajaunganisha WhatsApp akifungua WhatsApp inbox, ukurasa huo unapakia programu ya Meta (Facebook SDK) ili kufungua dirisha la kuunganisha. Anachoingiza kwenye dirisha hilo kinashughulikiwa na Meta chini ya sera yake ya faragha.
- Google (Marekani): muuzaji akitumia AI msaidizi, au mtu akiuliza kwenye chat ya duka au ya ukurasa wa mwanzo, ujumbe huo (bila namba za simu na barua pepe) pamoja na catalog ya duka au orodha ya maduka vinatumwa kwa Google (Gemini) ili kuandaa jibu. Tunatumia huduma ya bure ya Gemini: kwa masharti yake, Google inaweza kutumia taarifa hizo kuboresha huduma zake, na wakaguzi wake wanaweza kuzisoma. Kwa hiyo usibandike wala usiandike taarifa nyeti, kama namba za malipo au za kitambulisho.
- Google (kuingia): muuzaji akichagua "Endelea na Google", Google inajua kwamba anaingia kwenye WekaOrder, na inatuthibitishia utambulisho wake.
- Anthropic (Marekani): AI msaidizi ukiwekwa kutumia Claude badala ya Gemini, taarifa hizo hizo zinatumwa kwa Anthropic. Kwa masharti ya huduma zake za biashara, Anthropic haitumii taarifa hizo kufundisha AI yake.
Watoa huduma hawa wanazitumia taarifa kwa niaba yetu tu. Ukibonyeza link ya WhatsApp, Instagram, TikTok au Facebook, unaenda kwenye huduma hizo na sera zao za faragha zinahusika. Picha ya bidhaa iliyowekwa kwa link ya website nyingine inapakuliwa kutoka website hiyo.
Tunaweza kutoa taarifa pale tu sheria inapotulazimisha, kwa mfano kwa amri ya mahakama. Mamlaka ya serikali ikiomba taarifa za mtumiaji:
- Tunahakiki kwanza kama ombi ni halali kisheria na limekuja kwa njia rasmi.
- Ombi tunaloona si halali tunalikataa, au tunalipinga kwa njia za kisheria.
- Tukilazimika kutoa taarifa, tunatoa kiasi kidogo kabisa kinachohitajika.
- Tunaweka kumbukumbu ya kila ombi: nani aliomba, lini, tulijibu nini na kwa nini.
5. Taarifa zinahifadhiwa wapi na zinalindwaje
Server na database ya WekaOrder ziko Marekani (Railway, eneo la US East). Kwa hiyo taarifa zako zinahifadhiwa nje ya Tanzania.
Website inatumia HTTPS. Nenosiri linahifadhiwa kwa bcrypt, siri za MFA na token za WhatsApp zinahifadhiwa kwa encryption, na kila duka linaona taarifa zake tu. Unaweza kuwasha MFA kwenye "Akaunti yangu".
6. Tunazihifadhi kwa muda gani
- Taarifa za akaunti na duka zinabaki muda wote akaunti iko hai.
- Muuzaji akitenganisha WhatsApp kwenye WekaOrder, contacts za WhatsApp alizoleta zinafutwa mara moja. Mazungumzo yanabaki kwenye inbox ya duka hadi akaunti ifutwe.
- Ukifuta akaunti yako, inafutwa mara moja pamoja na duka, bidhaa, order (pamoja na taarifa za wateja), picha, code za punguzo, akaunti za wafanyakazi, mazungumzo ya customer care na muunganisho wa WhatsApp.
- Rekodi za malipo ya usajili (kiasi, tarehe, reference na jina la duka) zinabaki kwa miaka 5 kwa ajili ya kodi, kisha zinafutwa.
- Kumbukumbu za usalama zinabaki, lakini bila jina lako.
- Nakala za akiba (backups) zinaweza kubaki kwa hadi siku 30 kabla ya kufutwa.
- Link ya kubadilisha nenosiri inafanya kazi kwa dakika 30, na mwaliko wa mfanyakazi kwa siku 3.
- Anwani ya arifa ya kifaa inafutwa ukizima arifa au ukifuta akaunti.
- Alama za browsers 20 za mwisho ulizoingia nazo zinabaki hadi ufute akaunti. Hesabu ya nenosiri lililokosewa inafutwa ukiingia kwa nenosiri sahihi, au baada ya siku moja.
- Maelezo ya AI na majibu ambayo AI inajifunza yanafutwa muuzaji akiyafuta au akifuta akaunti.
8. Haki zako
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania (2022), una haki ya:
- kuomba nakala ya taarifa zako tulizonazo;
- kurekebisha taarifa zisizo sahihi (nyingi unaweza kuzibadilisha mwenyewe kwenye "Akaunti yangu" na "Duka langu");
- kufuta akaunti yako na taarifa zake;
- kupinga au kuzuia matumizi fulani ya taarifa zako;
- kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC).
Kama uliagiza kwenye duka na unataka taarifa zako zirekebishwe au zifutwe, wasiliana na muuzaji au na WekaOrder. Tutashirikiana na muuzaji kulishughulikia. Tunajibu kila ombi ndani ya siku 30.
9. Watoto
WekaOrder si huduma kwa ajili ya watoto. Akaunti ya muuzaji inapaswa kufunguliwa na mtu mwenye umri wa miaka 18 au zaidi.
10. Mabadiliko ya sera hii
Tukibadilisha sera hii, tutaweka tarehe mpya juu ya ukurasa huu. Kuhusu mabadiliko makubwa, tutawajulisha wauzaji kabla hayajaanza kutumika.
11. Wasiliana nasi
Kwa swali lolote kuhusu faragha, au kuomba taarifa zako, tuandikie:
- WhatsApp: 0749 356 109
- Barua pepe: billypatrick159@icloud.com