Kufuta akaunti ya WekaOrder

Jinsi ya kufuta akaunti

Huwezi kuingia?

Kama umesahau nenosiri, libadilishe kwanza kisha ufuate hatua zilizo juu.

Kama bado huwezi kuingia, tuma ombi la kufuta akaunti kupitia WhatsApp au barua pepe, ukitumia barua pepe au namba ya simu ya akaunti hiyo. Tutathibitisha kwamba akaunti ni yako na kuifuta ndani ya siku 30.

Kinachofutwa

Mwenye duka akifuta akaunti, vifuatavyo vinafutwa mara moja na haviwezi kurudishwa:

  • akaunti yako (jina, barua pepe, simu, nenosiri, MFA na arifa za simu);
  • duka na link yake, maelezo, picha na bidhaa zote;
  • order zote, pamoja na majina, simu na anwani za wateja;
  • code za punguzo na matangazo;
  • akaunti za wafanyakazi wa duka na mialiko yao;
  • mazungumzo ya customer care na WekaOrder;
  • muunganisho wa WhatsApp na ujumbe wake.

Kinachobaki, na kwa muda gani

  • Rekodi za malipo ya usajili (kiasi, tarehe, reference na jina la duka) kwa miaka 5, kwa ajili ya kodi.
  • Kumbukumbu za usalama kwamba duka lilifutwa, bila jina lako.
  • Nakala za akiba (backups) kwa hadi siku 30.

Wafanyakazi na wateja

Mfanyakazi akifuta akaunti yake, inafutwa akaunti yake tu. Duka na order zake zinabaki kwa mwenye duka, pamoja na jina lake kwenye malipo aliyothibitisha.

Wateja wanaoagiza hawana akaunti. Kama uliagiza na unataka taarifa zako zifutwe, wasiliana na muuzaji au na WekaOrder.

Kabla ya kufuta

Hifadhi taarifa unazohitaji, kama ripoti za mauzo, na uwajulishe wateja wenye order zinazosubiri. Baada ya kufuta, link ya duka lako haitafanya kazi tena.